Njombe

Wananchi wa mtaa wa Muungano halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamegomea kuuzika mwili wa kijana Elisha Nyalusi (35) wakidai kifo chake kimesababishwa na imani za kishirikina huku wakimtuhumu baba yake na kutaka arudishwe akiwa hai.

Wananchi hao akiwemo Nickson Nywage,Eliud Mwenda na Salima Mangula wamesema wamegomea kuuzika mwili huo kutokana na vijana wenzao wengine watatu kupoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha na kueleza kuwa vifo vyao vyote vimetokea tarehe za mwisho wa mwezi.

"Nadhani kulikuwa na mzozano wa shamba baadaye baba yake akamtuma akanunue dawa (roud up) ndipo alipodoka likimsokota tumbo kwa hiyo tumesusia kwasababu tumeumia yani sasa mwaka huu wametoka vijana wanne tayari kwa hiyo haturidhiki tunataka amrudishe tunaona vijana wenye nguvu wanapotea"wamesema wananchini

Hata Hivyo Baba wa kijana huyo aliyepoteza  maisha mwenye umri wa miaka 72  amekana kujihusisha na  Masuala ya imani za kishirikina na kueleza kuwa hakuwa na mgogoro wowote na mtoto wake kwani  na ndiye aliyekuwa akimtunza.

"Mtoto wangu tulishamalizana na alinunua shamba kwangu mbele ya mwenyekiti na shamba nilimkabidhi kwa hiyo tulikuwa hatuna changamoto yeyote na huyu mtoto wangu ndio aliyekuwa ananitunza"amesema baba Mzazi

Mwenyekiti wa mtaa wa Muungano Amelye Mteleke amekiri wananchi kugomea kuuzika mwili wa kijana huyo ambapo amesema tayari baba mzazi wa kijana huyo amechukuliwa na Polisi kwa ajili ya usalama wake.

"Inaonekana kuna maneno ya uchochezi yanayoashiria ushirikina amekuwa akiyatamka kwa hiyo vijana wote pamoja na wazee wamekasilishwa wakasema sasa we mzee utazika mwenyewe na familia yake inamtuhumu kwamba ni mshirikina"amesema Mteleke.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wakandarasi wazawa waliopewa dhamana ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliji kuhakikisha waaitekelza kwa weledi na ubora wa hali ya Kuu.

Majaliwa Ameyasema hayo Jana katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliaji katika maeneo mbalimbali, iliyofanyika jijini Dodoma.

"Ndugu washiriki nimefurahishwa kuona kuwa asilimia 82 ya wanaokwenda kujenga miradi hii ni wataalamu na hizi ni fursa za ajira kwa Watanzania, lakini ni fursa ya kuongeza ujuzi kupitia miradi hii, vilevile inakwenda kuongeza kipato kwa Watanzania.

"Nitoke rai kwa wakandarasi wazawa, kwanza mbadilike, mnathaani kubwa mmepewa ya kutekeleza miradi na hili ndicho kilio kikubwa cha private seckta (sekta binafsi) leo mmeona serikali imeendelea kutekeleza kwa kuwapa miradi.

"Mjipange vizuri tumieni fursa hii kuihakikishia serikali kwamba mnaweza, lakini nyie mna dhamira zenu kufungua kampuni za ukenzi, mna hiyo dhamira simamieni dhamira zenu. Sisi tunakutegemeeni nyie kufua milango ya ajira.



Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama (wa pili kushoto mstari wa pili) na Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi wa Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Hussein (kushoto) wakiwa katika maandamano ya wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja vya Jamhuri, jijini Dodoma yakiwa na kaulimbiu ya “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, (katikati) akiongoza maandamano ya watumishi wa Wizara hiyo wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja vya Jamhuri, jijini Dodoma, yakiwa na kaulimbiu ya “Nyongeza ya mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Watumishi wa Wizara ya Fedha wakipita kwa bashasha mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule, ambaye alikuwa mgeni rasmi wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja vya Jamhuri, jijini Dodoma, yakiwa na kaulimbiu ya “Nyongeza ya mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Bw. Mbayan Saruni (katikati) akiteta jambo na baadhi ya watumishi walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja vya Jamhuri, jijini Dodoma, yakiwa na kaulimbiu ya “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Watumishi wa Wizara ya Fedha wakiwa tayari kuanza maandamano kuelekea Viwanja vya Jamhuri, jijini Dodoma kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja hivyo, jijini Dodoma, yakiwa na kaulimbiu ya “Nyongeza ya mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha wakiwa wakiwa tayari kushiriki Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja Viwanja vya Jamhuri, jijini Dodoma, yakiwa na kaulimbiu ya “Nyongeza ya mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha wakiwa katika maandamano wakati wa  Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja vya Jamhuri,  jijini Dodoma, yakiwa na kaulimbiu ya  “Nyongeza ya mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha wakifurahia jambo wakati wa  Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa katika Viwanja vya Jamhuri,  jijini Dodoma, yakiwa na kaulimbiu ya  “Nyongeza ya mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha- Dodoma)

 Katika kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), leo tarehe 01 Mei, 2024 imetembelea Kituo cha Watoto wenye uhitaji cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali.

Akikabidhi msaada huo  kwaniaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Afisa Habari Mkuu Bi. Christina Njovu alieleza kuwa Wakala imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera  ya kurudisha kwa jamii ambapo wakala imekuwa ikiitekeleza mara kwa mara.

Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vyakula vikiwemo unga, sukari,vifaa vya usafi na vifaa vya shule 

Naye Mkuu wa Kituo cha CHAKUWAMA  Bw. Hassan Hamis ameishukuru BRELA kwa kufika kituoni hapo kuwatembelea na kwa msaada uliotolewa ambao umewapa faraja kubwa ikizingatiwa kwamba hivi karibuni wamepatwa na janga la moto kwa kuunguliwa na bweni la kulala Watoto.

Aidha Bw. Hamis ameeleza kuwa, Kwa sasa kituo kina watoto 72 wa jinsia zote wenye umri tofauti kuanzia chini ya mwaka mmoja hadi miaka 19 na wengi wao wanasoma shule ya msingi na sekondari na kwamba changamoto zao ni nyingi hivyo ujio wa BRELA na vifaa ilivyotoa vitapunguza ukali wa  baadhi changamoto zinazowakabili.

Akielezea historia ya kituo hicho Bw. Hamis.amesema kuwa, Kituo kilianza mwaka 1998 kikiwa na Watoto 5 chini ya mwanzilishi Bi. Saida Hassan kikitumia nyumba ya kupanga eneo la Mikocheni ,  Kituo kimesajiliwa na kinafanya kazi kwa karibu na Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia Watoto na makundi maalum.

Na kuongeza kuwa kituo kina watoto aliowatenga katika  makundi sita wakiwemo,  yatima waliopoteza wazazi wote wawili,  Watoto waliopoteza mzazi mmoja, wapo waliotolewa kwenye mazingira hatarishi na wale waliofanyiwa ukatili na walio okolewa kutoka biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu pamoja na walemavu. 

Katika Watoto 72 watoto 60 wanasoma katika ngazi tofauti kuanzia chekechea, msingi, sekondari, veta na vyuo  katika  shule za serikali na shule binafsi za kulipia. 

Aidha Bw.Hamis ameeleza kuwa moja ya changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na Watoto 12 wamesimamishwa kuendelea na masomo kutona na kuathilika kiakili kulikotokana na ukatili waliofanyiwa na wengine kupata magonjwa na hivyo wanaendelea na matibabu. 

Mbali ya kutembelea kituo cha Watoto wahitaji, BRELA pia imeshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyobebwa na kaulimbiu Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga dhidi ya hali ngumu ya maisha.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi na Wafanyakazi kutoka Wizara, Taasisi za Serikali na Binafsi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.

Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta Binafsi wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Gazeti la Mfanyakazi Tanzania wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024. Kushoto ni Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Tumaini Nyamhokya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha Gazeti la Mfanyakazi Tanzania mara baada ya kulizindua wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa zawadi ya ujumla kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambao wameongoza katika michezo mbalimbali katika kuadhimisha ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mkoani Arusha tarehe 01 Mei 2024.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kuhakikisha fedha zinazotolewa na kampuni hiyo kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii (CSR) zinagusa na kubadilisha maisha ya wananchi wa mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujumla.

Mbali na kuipongeza GGML kwa kuja na tenolojia mbalimbali za uokoaji katika maonesho ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) yanayoendelea kwenye viwanja vya General jijini Arusha, pia alieleza kuridhishwa na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu masuala ya afya na usalama mahali pa kazi.

Makonda ambaye alitembelea banda la GGML katika maonesho hayo jana alisema mara nyingi maisha ya watu wa Geita hayafanani na utajiri uliopo katika mkoa huo.

“Mimi sioni aibu kuitwa tajiri,kwa sababu hilo ni jambo la Kujivunia hivyo siwezi kujivunia umaskini ndio maana nataka ninyi Watanzania mliopo kwenye mgodi huu kuendelea kuwa chanzo cha mabadiliko ya watanzania wenzenu wanaozunguka mgodi huu,” alisema.

Aidha, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi alimpatia maelezo Makonda kwamba mpango wa CSR wa mwaka huu ni mwendelezo wa mipango ya awali unaolenga kujumuisha maendeleo yaliyofikiwa na GGML hadi sasa katika maeneo ya mazingira, miundombinu, afya, elimu na biashara ndogondogo na za kati (SMEs) katika jamii ya mwenyeji wa Geita.

Dk. Kiva alitoa mfano kuwa mwaka jana GGML imesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na wenyeji wake Halmashauri ya Mji Geita, Wilaya ya Geita pamoja na Halmashauri za jirani za wilaya za Chato, Bukombe na Mbogwe kutekeleza Mpango wa Uwajibikaji wake kwa Jamii (CSR) kwa mwaka 2022/2023 wenye thamani ya Sh bilioni 19.

“Jumla ya Sh bilioni 9.8 zilitengwa kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, bajeti ya Sh bilioni 8.6 ilitengwa.

“Uwepo wa GGML katika mkoa wa Geita umeonyesha matokeo chanya katika sekta ya elimu baada ya kampuni hiyo kujenga miundombinu zaidi ya 1800 ya shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Geita yenye halmashauri mbili za Geita mji na ile ya wilaya ya Geita,” alisema.

Alisema miundombinu hiyo imetokana na utekelezaji wa mabadiliko ya sheria ya madini ya mwaka 2017 ambapo GGML imekuwa ikiandaa mpango wa huduma kwa jamii kwa kushirikiana na halmashauri husika huku kila mwaka hutenga kiasi cha Sh 9.2 bilioni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mbali na miradi ya elimu, Dk. Kiva alisema GGML kupitia fedha za CSR walitenga fedha kwa ajili ya miradi ya mazingira ambapo kiasi cha Sh700 milioni zinatumika.

“Ipo pia miradi ya kimkakati ukiwemo ule wa ufugaji wa samaki, miradi kwa kinamama na vijana pamoja na wasiojiweza ambapo zaidi ya Sh1.5 bilioni zinatumika.

Alisema miradi hiyo inaongeza thamani katika sekta mbalimba za kiuchumi na kuwapatia wananchi maendeleo.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira wa GGML, Dk Kiva Mvungi (kulia) wakifurahia jambo katika banda la GGML wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha. Katika Maonyesho ya OSHA 2023, Geita Gold Mining ilitambuliwa kama kampuni iliyofanya vizuri zaidi katika masuala ya afya na usalama kazini, na pia ilitunukiwa tuzo ya muonyeshaji bora kwa ujumla.

Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu leo tarehe 1 Mei, 2024 wameshiriki maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) yaliyofanyika kimkoa katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 1 Mei ambapo kwa mwaka huu kitaifa yamefanyika Jijini Arusha na Mgeni Rasmi alikuwa Makamu ya Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.






Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais ,Mary Maganga (wa pili kulia) wakikabidhi tuzo ya ushindi wa Jumla kwa wafanyakazi wa Barrick (kutoka kushoto) ni Hassan Kallegeya Safety Coordinator (Bulyanhulu) na kulia ni Aristides Medard (Specialist Occupational Hygiene, Katika hafla iliyofanyika jijini Arusha. Mbali na ushindi wa Jumla Barrick imeshinda tuzo nyingine 4

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nicolaus Mkapa, akimkabidhi tuzo kwa ushindi wa kwanza katika sekta ya madini kwa Mtaalamu wa masuala ya Usalama wa Barrick –Specialist Occupational Hygiene, Aristides Medard katika hafla ya kukabidhi tuzo iliyofanyika jijini Arusha. Wengine pichani ni Wafanyakazi wa Barrick. Mbali na ushindi wa Jumla Barrick imeshinda tuzo nyingine 4.






Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo ambazo kampuni imejishindia.


Na Mwandishi Wetu.


Barrick Tanzania imenyakua tuzo tano katika hafla ya utoaji wa tuzo za Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ya 2024 iliyofanyika jijini Arusha ambapo Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, umeshinda tuzo kubwa ya mshindi wa juu wa Jumla katika Tuzo ya Afya na Usalama (OHS) 2024.

Mbali na ushindi huo mkubwa, Bulyanhulu, pia ilinyakua tuzo za Utawala Bora ofisini, usaidizi wa kiofisi na shughuli za ukuzaji biashara , na mshindi Bora wa Ubunifu kwenye maonyesho ya OSHA ya mwaka huu kwenye sekta ya madini.

Kwa upande wake, Barrick North Mara ilishinda tuzo ya juu katika Kuwajali Zaidi Wafanyakazi wenye Mahitaji Maalum.

Maonyesho ya OSHA mwaka huu yalifanyika katika viwanja vya General Tyre jijini Arusha, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwaka huu ambapo aliwakilishwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Patrobas Katambi.

Barrick Tanzania imeshinda tuzo za 2024 kutokana na mafanikio ya 2023 ya kampuni ambapo ilishinda tuzo ya jumla ikiwemo tuzo za uandaaji Ripoti Bora ya Tathmini ya Hatari katika uchimbaji madini na mshindi Bora wa tuzo ya Usalama na afya (OHS) katika sekta ya madini.

Tuzo nyingine ilizoshinda zilikuwa ni Kujali zaidi Wafanyakazi wenye Mahitaji Maalum na utekelezaji sera bora ya Usalama mahali pa kazi (OHS), mshindi wa pili kwa washindi wa jumla wa sekta ya Madini, utekelezaji Mpango Kazi Bora wa Usalama na Afya mahali pa kazi.

Usalama ni sehemu muhimu ya DNA ya Barrick. Kampuni ina mpango maalum kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wake na wakandarasi, kuhakikisha kwamba kila mtu anarudi nyumbani akiwa na afya njema na salama. Juu ya yote hayo katika Barrick kila mtu amejitolea kufanya a kuhakikisha hakuna matukuo ya ajali katika sehemu yake anapofanyia kazi.

Katika maonesho ya mwaka huu Barrick pia ilifiikisha elimu ya afya na usalama kwa wananchi waliotembelea kwenye banda lake kwenye maonesho haya sambamba na kushiriki zoezi la kupanda miti katika kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya maonesho ya athari za mabadiliko ya tabia nchi katika usalama na afya kazini:sajili eneo lako la kazi OSHA katika harakati za kupunguza athari hizo.

Na Mwandishi Wetu 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)  imesema uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya Mtwara kunatarajiwa kusababisha uwepo wa vipindi vikubwa vya mvua katika  baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro, Dar es Salaam na maeneo ya jirani.

Katika taarifa iliyotolewa  na Mamlaka hiyo, leo Mei Mosi, 2024 inasema, mifumo ya hali ya hewa iliyopo kwa sasa inaonesha kuwa mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kuimarika na kufikia hadhi ya Kimbunga kamili hadi kufikia kesho, Mei 2 2024.

"Wakati mgandamizo huo mdogo wa hewa ukiendelea kuimarika, unatarajiwa pia kusogea kuelekea baadhi ya maeneo ya pwani ya nchi yetu kuanzia usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa, Mei 3, 2024 na kwamba Mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kuendelea kuwepo katika maeneo ya ukanda wa pwani ya nchi  hadi  Mei 6, 2024". Imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Imeendelea kuelezwa kuwa, Hata hivyo, mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kupungua nguvu baada ya Mei 6 2024.

Taarifa hiyo imesema, uwepo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa unatarajiwa kutawala na kuathiri mifumo ya hali ya hewa hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro, Dar es Salaam na maeneo ya jirani. 

Hata hivyo, Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo mdogo wa hewa na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa mara kwa mara kila inapobidi.




Na Derek MURUSURI, Dodoma


SHIRIKA la Utangazaji Tanzania litaendelea kutoa fursa sawa kutangaza kampeni za vyama vyote vitakavyoshiriki uchaguzi wa mwaka huu na mwaka 2025.

"Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, TBC ilifuata ratiba ya kampeni ya vyama vya siasa, na kwingine TBC walifika na vyama vyenyewe havikufika," alisema Mhandisi Andrew Kisaka, Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano cha TCRA.

Mhandishi Kisaka alikuwa akijibu hoja ya Mwanahabari na Mkuu wa Wilaya Mstaafu, Jenerali Ulimwengu.

Mwanahabari huyo, aliitaka TBC isichukue matangazo ya biashara kwa vile inafadhiliwa na Serikali na kuwataka watoe fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu.

"Ni kweli TBC ni Shirika la Utangazaji la Umma na linaendelea kuchukua matangazo kwa sababu bado funding (ufadhili) yake haijakidhi viwango vya kuwa public broadcaster, lakini funding yake inafanyiwa kazi," alisema Mhandisi huyo.

Mhandisi Andrew Kisaka alisema hayo katika Kongamano la siku moja la wadau wa Habari na Uchaguzi, lililoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) katika Hoteli ya Dodoma jana (30 April, 2024).

Katika Uchaguzi wa mwaka 2020, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waliwafukuza TBC katika mkutano wao wa kampeni.



Madhumuni


Akielezea madhumuni ya Kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa MCT, Bw Ernest Sungura, alisema kuwa waliwaleta pamoja wadau wa habari ili kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja katika kuongeza uwazi, haki na uwajibikaji tunapoelekea katika chaguzi za mwaka huu na 2025.


"Dira ya MCT ni kuchangia ukuaji wa demokrasia ya Tanzania kupitia uchaguzi wa viongozi kwa sanduku la kura na kujenga jamii ya haki," alisema Bw Sungura.

Manufaa ya Kongamano

Kongamano hilo lililofadhiliwa na Ubalozi wa Marekani nchini pamoja na Shirika la Kimataifa linalohusika na masuala ya Uchaguzi (IFES), lilikuwa na manufaa manne.

Kwanza ni kukuza maadili ya kidemokrasia kutokana na kujenga misingi ya
HAKI, UWAZI na UWAJIBIKAJI.

Pili, ni kuimarisha uhuru wa kutoa maoni kupitia
vyombo vya habari.

Manufaa mengine ni kuongeza elimu kwa wapiga kura itakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi namakini katika sanduku la kupiga kura.

Mwisho, Bw Sungura alisema ni kuimarisha ushirikiano na kuaminiana miongoni mwa wadau muhimu wa uchaguzi.

"Hii ni pamoja na kuongeza imani kwa umma kutokana na
uandishi wa Habari usioficha kitu na usioegemea upande mmoja, unaotoa taarifa sahihi na za ukweli," alisisitiza.

Kongamano hilo la kwanza kufanyika nchini, lilihudhuriwa na washiriki mbalimbali kutoka vyombo vya habari pamoja na wadau wa Habari na uchaguzi.

Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi.



Na Mwandishi Wetu,DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imewaahidi watanzania kuwepo kwa Uchaguzi Huru na Haki ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu mwakani huku ikisisitiza kila mtu atapata haki yake ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa bila kuwepo kwa vihatarishi vya amani katika maeneo yote ambapo chaguzi hizo zitafanyika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati akihojiwa na waandishi wa Habari baada ya kufungua Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,Msalato jijini Dodoma huku akisisitiza kuboreshwa na kuwepo kwa ongezeko la bajeti ambalo halijapata kutokea ambapo kikao hicho kilihudhuriwa pia na Wakuu wa Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo.

‘Niwahakikishie wananchi tumejipanga vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani,niwaombea watanzania watege masikio kuelekea bajeti ya wizara ambayo tutaiwasilisha bungeni katikati ya mwezi unaokuja,tunaenda kuboresha takribani kila sehemu katika vyombo vyetu vya usalama hasa Jeshi la Polisi tunaenda kuliboresha katika kila sehemu ikiwemo vifaa na mambo mengine mbalimbali.’ Alisema Masauni

Akizungumzia zaidi uchaguzi Waziri Masauni amesema wananchi wasiwe na wasiwasi serikali kupitia vyombo vya usalama kupitia Jeshi la Polisi iko vizuri kwa namna yoyote ile kuhakikisha kwamba demokrasia inaendelea kutekelezwa katika misingi ya amani na utulivu,watu wanachagua na kuchaguliwa bila bughudha yoyote nan chi itaendelea kubakia salama katika maeneo yote.

Akizungumzia Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Camillus Wambura amesema anampongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni kwa kusimamia ongezeko la bajeti kwa wizara na vyombo vyake ambapo ongezeko hilo linaenda kuboresha utendaji kazi hasa wa jeshi la polisi kuelekea pia uchaguzi wa Serikali za Mita ana Uchaguzi Mwakani.

‘Mwaka huu tunakwenda kuingia kwenye uchaguzi na mwaka kesho uchaguzi mkuu,wizara yetu ina nafasi kubwa sana kuhakikisha uchaguzi unakua wa huru na wa haki kwahiyo niwaombe wajumbe kutambua kwamba hii ngoma bado ni ya kwetu na mpiga ngoma ni Mheshimiwa Waziri kwahiyo tukae tayari kucheza ngoma hiyo ili kuhakikisha chaguzi zote mbili zinapita salama’ alisema IGP Wambura

Mkutano huo wa Baraza la Wafanyakazi uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu ambapo mambo mbalimbali kuelekea Bajeti Kuu ya Wizara itakayowasilishwa bungeni katikati ya mwezi ujao yalijadiliwa huku Katibu Mkuu akiwataka watumishi kuwa wabunifu,waadilifu na kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassani ya utolewaji wa huduma sahihi na zisizo na upendeleo kwa wananchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) akiimba wimbo wa mshikamano pamoja na viongozi, watumishi wa wizara (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,Msalato jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,Msalato jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,Msalato jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Ally Senga Gugu akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,Msalato jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Dkt.Maduhu Kazi akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,Msalato jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
WATUMISHI wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)leo Mei Mosi 2024 wameungana na Wafanyakazi Duniani kote kuadhimisha Siku yao adhimu ambapo kitaifa maadhimisho yanaendelea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijinu Arusha na Mgeni Rasmi wa Sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango


TAWIRI tunajivuni mchango mkubwa wa watumishi katika kusimamia, kuratibu na kufanya tafiti za wanyamapori nchini kwa ustawi wa uhifadhi na kukuza utalii nchini.

Aidha, Kauli mbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu ni *"Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha"*







Top News